Man utd yaamka usingizini, yaichapa Sunderland 3-0.


Baada ya kuvuna sare mbili mfululizo hatimaye Manchester United imeng'oa pointi 3 katika uwanja wa Light baada ya kuichapa Sunderland bao 3-0.

Mabao ya Man utd yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan pamoja na Marcus Rashford ambaye alihitimisha ubao wa mabao 3.

Ushindi huo unaisogeza Man utd kwenye nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi kuu England baada ya kukusanya jumla ya pointi 57.

Comments