Man utd yakabwa koo na Everton Old Trafford.


Timu ya Manchester United imepata sare kwa mara ya pili mfululizo katika uwanja wa Old Trafford baada ya kuchomoa bao na kuyafanya matokeo kuwa 1-1 dhidi ya Everton.

Man Utd walitoka sare na West Brom Albion jumamosi ya wiki iliyopita na imelazimishwa sare pia na Everton hapo jana.

Everton ilipata bao la kuongoza kupitia Phil Jagielka aliyefunga kipindi cha kwanza hata hivyo Man Utd ilichomoa bao hilo kupitia Ibrahimovic aliyefunga kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 90.

Comments