April 22, 2017
Timu ya Manchester itamaliza msimu huu na kuanza msimu mpya wa ligi 2017/18 mwezi Agosti bila mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovic.
Zlatan mwenye miaka 35 aliumia kwenye mechi ya Europa ligi dhidi ya Anderlecht baada ya kuruka na kutua chini ambapo mguu wake wa kulia ulitua vibaya na kupinda sehemu ya nyuma.
Mshambuliaji huyo amekuwa muhimu katika timu hiyo tangu alipotua Old Trafford mwaka jana na tayari ameifungia Man utd jumla ya magoli 28.
Raia huyo wa Sweden atasherekea kupokea umri wa miaka 36 mwezi Oktoba mwaka huu akiwa nje uwanja.

Comments
Post a Comment