Manara ainyea TFF ya Malinzi.


Msemaji wa klabu ya Simba amemwambia Rais TFF Jamal Malinzi kijiuzulu kwenye wadhifa wake kutokana na uendeshaji mbovu wa shirikisho hilo.

Uongozi wa Simba kiujumla umemtaka Malinzi kuachia ngazi nafasi ya urais ili akatumike nafasi ya uenyekiti wa chama cha soka mkoani kagera.

Simba kupitia Haji Manara wamesema kuwa Rais huyo ameshindwa kulitendea haki suala la rufaa ya yao ambayo kama saa 72 ilikuwa imekwisha toa maamuzi.

Pia Manara ameituhumu kamati inayosimamiwa na katibu wa TFF celestine Mwesigwa kutokana na kuipinga kamati ya saa 72 kutokana na kila kitu kuwa wazi.

"Tumechoka kudhulimiwa na kuonewa, nasi tunataka haki itendeke, TFF wanakiwa kuachana na dhuluma na kuitazama haki ilipo kwa kuwa imeshafahamika kuwa Mohamed Fakhi ana kadi 3 za njano.

"Kwa wazi kabisa mtu anaona haridhishwi ma hukumu iliyotoka anaamua kuunda kamati ya nyingine ili kupindisha suala letu." Alisema Manara

Comments