Mane kuikosa Bournemouth kesho.


Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane atakosa mchezo wa kesho dhidi ya AFC Bournemouth kutokana na jeraha la goti.

Mane aliumia goti katika mechi ambayo Liverpool ilipata ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Everton ambapo hakuweza kumaliza dakika 90 licha kufunga kwenye mechi hiyo.

Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha taarifa za kukosekana kwa mchezaji huyo alipokuwa kwenye mkutano na waandishi habari.

"Jordan Henderson, Adam Lallana na Sadio Mane wataukosa mchezo lakini Daniel Sturridge amerejea na kuanza mazoezi na timu." Alisema

Comments