Timu ya Liverpool imepata pigo jingine ambapo itamkosa nyota wao Sadio Mane kwa kipindi chote kilichobaki msimu huu.
Hayo yemethibitishwa na meneja wa Liverpool Jurgen Klopp baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wataalam wanaoshughurikia tatizo la Sadio Mane.
Mane alishindwa kuendelea katika mechi ambayo Liverpool ilipata ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Everton baada ya kuumia goti na nafasi yake ilijazwa na Divock Origi aliyeingia dakika ya 57 ya mechi hiyo.
"Mane atafanyiwa upasuaji na hatufahamu, itakuwa lini ukweli ni kwamba atakosa kipindj chote cha msimu huu." Alisema Jurgen Klopp
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal amekuwa nguzo katika timu hiyo tangu asajiliwe kwa dau la £34 milioni akitokea Southampton, na kuweza kuifungia Liverpool mabao 13 msimu huu hiyo ikiwa ni kwenye ligi kuu pekee.

Comments
Post a Comment