April 26, 2017
Timu ya Mbao FC imetamba kumuondoa Yanga kwenye hatua ya nusu fainali na kutinga kwenye fainali ya kombe la FA.
Mbao imetamba kuwa itajipanga vema kuidhibiti safu ya ushambuliaji ya Yanga akiwemo Amis Tambwe, Obrey Chirwa na Simon Msuva.
Akizungumza kwa kujiamini msemaji wa timu hiyo Chrisant Malinzi alisema wamejipanga vizuri kumuondoa Yanga na wamefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha Tambwe na Msuva hawafurukuti kwenye mchezo huo.
"Tulianza vizuri tangu mwanzo kuweka mikakati iliyo bora hadi tumefika tumefika nusu fainali.
"Kikosi chetu kina maandalizi ya kutosha tumejipanga imara kwenye safu ya ulinzi kuwathibiti Amis Tambwe na Simon Msuva." Alisema Malinzi
Mbali na mchezo huo utakaopigwa jumapili ya wiki, Simba na Azam ndiyo watakaoanza katika nusu ya kwanza ambayo itachezwa jumamosi katika uwanja wa taifa.

Comments
Post a Comment