Ahadi iliyotelewa na Mbao FC imetimia baadaya ya kuichomoa Yanga kwenye nusu fainali ya kombe la FA baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Awali Mbao FC kupitia msemaji wake Chrisant Malinzi ilitoa ahadi ya kuichomoa Yanga kwenye hatua hiyo kutokana na maandalizi mazuri waliyokuwa nayo.
Bao la Andrew Vicent 'Dante' aliyejifunga ndilo lililoipeleka Mbao FC katika fainali ya kombe la FA.
Mbao na Simba ndiyo watakaocheza mchezo wa fainali na kumsaka mwakilishi wa michuano ya kimataifa katika michuano ya kombe la Shirikisho.

Comments
Post a Comment