Messi aimaliza Real Madrid Santiago Bernabeu.


Mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi ameweka rehani ubingwa kwa timu ya Real Madrid baada ya kufunga bao 2 kwenye ushindi  3-2 walioupata Santiago Bernabeu.

Messi alifunga bao hizo katika dakika ya 33 na lingine katika dakika ya 90 na kuinyanyua Barcelona juu ya msimamo wa ligi ya Hispania.

Barcelona na Real Madrid zimefungana kwa jumla ya pointi 75 kwenye msimamo wa ligi lakini bado Real Madrid ina mchezo mkononi.

Mbali na ushindi huo, pia Real Madrid ilipata pigo baada ya Sergio Ramos kulimwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 78 ya mechi baada ya kumchezea vibaya Lionel Messi.

Comments