Mshahara wamwondoa Chirwa kikosini.


Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa hayupo kwenye orodha ya wachezaji waliosafiri kuelekea Algeria baada ya kukosa malipo ya mshahara wa mwezi mmoja.

Mchezaji huyo aligoma kutoa hati yake ya kusafiria kutokana na Yanga kukwama kumlimpa mshahara wake licha ya umuhimu alionao kwenye kikosi hicho.

Hata hivyo kulingana na majibu ya katibu mkuu wa Yanga Bonifasi Mkwasa alisema kuwa kocha wa timu hiyo George Lwandamina aliliridhia kusafiri na kikosi hicho bila nyota huyo.

Pia Lwandamina alisema kuwa timu haina ulazima wa kumtegemea nyota mmoja licha ya kuwa muhimu kwenye kikosi cha Yanga msimu huu.

Yanga ilipata ushindi katika mchezo wa nyumbani baada ya kuilaza MC Alger bao 1-0 kwa sifuri na hivyo itakuwa na kibarua kizito cha kutetea na kulinda nafasi kwenye mchezo marudiano.

Comments