Ngoma aondolewa kikosi kuivaa Mbao FC.


Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma hajausishwa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoivaa Mbao FC kwenye nusu fainali ya kombe la FA.

Yanga itacheza mechi ya nusu fainali ya michuano hiyo Jumapili ya wiki hii katika uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Mbao FC.

Mbali na Donald Ngoma wengine walioachwa ni pamoja na mshambuliaji Malimi Busungu pamoja na beki Vincent Boussou.

Comments