Ngoma yupo fiti kuivaa MC Alger.


Mshambuliaji wa Yanga SC Donald Ngoma amerejea uwanjani baada ya kupona jeraha lake la goti lililokuwa linamkabili.

Ngoma alianza mazoezi mepesi wiki mbili zilizopita na sasa amepona kabisa na atakuwa  tayari kusakata kabumbu katika mchezo katika raundi ya mtoano dhidi ya MC Alger ya Algeria.

Raia huyo wa Zimbabwe alianza kusua kusua katika soka tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara ambapo mara nyingi amekuwa akikosa mechi muhimu kutokana na majeraha.

Kupona kwa Donald Ngoma ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga ambao wana matumaini makubwa ya kutetea ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Kurejea kwa Donald Ngoma kutaongeza nguvu kubwa kwenye safu ya Mshambuliaji wa Yanga ambayo imekuwa ikisukumwa zaidi na Simon HappyGod Msuva pamoja na Obrey Chirwa.

Comments