Ni mwaka wa shetani kwa Arsenal, yapigwa bao 3-0 na Crystal Palace.


Inawezekana huu ukawa ndiyo msimu mbaya zaidi kwa Arsenal kwa zaidi miaka 20 iliyopita baada ya kupigwa mabao 3-0 na Crystal Palace ambayo nayo inapatikana London.

Arsenal imebaki nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi kuu England baada ya kipigo hicho ikiwa chini ya Manchester United ambayo ilishinda mechi yake dhidi ya Sunderland.

Huu ni mwenendo mbaya kwa Arsenal ambayo huenda ikashindwa kuingia kwenye nne bora kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu.

Comments