Wabingwa watetezi wa ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama 'league 1' Paris Saint Germain (PSG) imeonesha dalili ya kujivua ubingwa baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Nice.
PSG imecheza jumla ya michezo 35 kwenye ligi kuu na kukusanya kumla ya pointi 80 juma ya Monaco yenye pointi 83 na mchezo mmoja mmoja mkononi.
Mabingwa hao watetezi walishindwa kuthibitisha ubora wao mbele ya Nice ambao walianza kuchungulia mlango wa mabao wakiongozwa na Mario Balloteli.
Aidha PSG imepata hasara ya kuwapoteza nyota wake wawili Angel Di Maria pamoja na Maria Thiago Motta ambao walioneshwa kadi nyekundu katika dakika ya 90 ya mechi hiyo.
Endapo Monaco itashinda michezo yake miwili ifuatayo itakuwa imejihakikishia kumpoka ubingwa PSG na kuwa bingwa mpya baada ya misimu 6.

Comments
Post a Comment