Mbali na mechi ya Simba na Mbao FC leo kutakuwa na mtanange mwingine ligi kuu Vodacom katika ya Azam na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Mtibwa Sugar ndiye mwenyeji wa mchezo huo ambao utapigwa majira ya saa 10 za jioni ukiwa ni mchezo wenye ushindani wa aina yake.
Azam inaweza kuwa yenye kujiamini zaidi kutokana na rekodi nzuri aliyonayo dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo mpaka sasa wameshakutana mara 17.
Tangu mwaka 2008 ambapo Azam ilipanda daraja na kutinga ligi kuu Tanzania bara imeshinda mara 9 dhidi ya Mtibwa, zikiwa zimetoka sare mara 6 na Azam ikifungwa mara 2.
Pia Azam imeweza kushida mara nyingi ugenini, hadi sasa imeshinda mara 5 katika uwanja wa Manungu, na kufungwa mara moja pamoja na sare moja.
Rekodi inaonekana kuinyanyua Azam dhidi ya Mtibwa Sugar, lakini si matokeo ya dakika 90 katika mchezo wa leo yanaweza kunyanyua rekodi hizo.
Mchezo wa soka upo kwenye mabadiliko makubwa kulingana na wakati na ubora wa kikosi cha timu husika licha ya rekodi na historia zilizopo.
Ingawa kitaalam tunaweza kushuku na kuamini huenda Azam ikatoka na pointi 3 katika mchezo wa leo kutokana na uhalisia wa takwimu zilizopo.
Nina imani mchezo utakuwa wa aina yake na wenye kujawa na ushindi, imani inaniambia atakayekuwa kwenye ubora kuliko mwingine basi atachomoka na pointi 3 za mechi hiyo.

Comments
Post a Comment