Sanchez kuibua vita ya karne EPL.


Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez huwa huenda akaibua ushindani mzito wa usajili katika timu 3 kubwa za England.

Manchester United, Manchester City pamoja na Chelsea zote zimeonesha nia kumwania mchezaji huyo ambaye alitangaza kutimka Arsenal mwisho wa msimu huu.

Licha ya Conte kuwasilisha jina la mchezaji huyo kwenye orodha ya wachezaji anaotaka kwa Roman Abromovic lakini atakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Jose Mourinho na Pep Gurdiola.

Mourinho anataka kufanya mageuzi kwenye safu ya ushambuliaji ili kuirejesha Man utd kwenye hadhi na kuleta mataji Old Trafford na raia huyo wa Chile ameingia kwenye mipango yake.

Hali inaweza kuwa ya ushindani zaidi endapo makocha wote hao wataingia kwenye mbio za kumwania nyota huyo.

Comments