Simba kuipeleka TFF, FIFA?


April 25, 2017

Uongozi wa Simba SC huenda ukapeleka malalamiko yao FIFA baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya TFF kuhusiana na kupokwa pointi tatu za Kagera Sugar.

Hayo yaliwahi kuwekwa wazi na msemaji wa Simba Haji ambaye kwa sasa amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka.

Simba kupitia msemaji huyo iliwahi kusisitiza endapo wataikosa haki yao kupitia TFF basi watadai haki hiyo ngazi za juu.

Awali Manara alikaririwa kuiponda kamati ya katiba, sheria na hadhi ya wachezaji akidai kuwa haikuwa na haki ya kuingilia maamuzi yaliyokwisha tolewa na kamati ya saa 72.

Kuna kila dalili huenda Simba ikatinga ngazi za juu kupigania suala wakidai kuonewa na uongozi wa TFF chini ya Rais wao Jamal Malinzi.

Comments