Ni mchezo wa aina yake wenye kusubiriwa kwa hamu kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania, wakiwemo mashabiki wa wenye asili ya paka na panya yaani Simba na Yanga.
Tayari Simba ilipoteza pointi 3 katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera baada ya kupokea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar.
Simba ina kazi ngumu ya kuikabili Mbao FC ambayo ni kati ya timu yenye mipango iliyokamaa katika namna ya kumkabili aina ya mpinzani wanayekutana naye.
Ikumbukwe kuwa Mbao FC ni moja kati ya timu zenye mbinu kali za kumkabili mpinzani wanayekutana nae uwanjani, hivyo haishangazi kama Azam ilikufa pale kirumba kwa baada kufungwa bao 4-0 na wababe hao wa mwanza.
Naukumbuka ule mpango kabambe ambao uliiwezesha Mbao FC kuing'oa Kagera Sugar ambayo ilikuwa kwenye uwanja wa nyumbani katika mchezo wa robo fainali ya kombe la FA ambao Mbao FC ilishinda bao 2-1.
Ikumbukwe Mzamiru Yasin ndiye aliyeipatia Simba bao la pekee la ushindi pale taifa zikiwa zimesalia dakika 3 katika muda wa dakika za nyongeza.
Kwa mtazamaji wa soka atakubaliana nami kuwa Mbao FC ni moja kati ya timu nzuri na imara ambazo zimepata kutokea msimu huu, uwezo na mbinu zao ndizo zilizoipa tabu Simba katika mchezo wa kwanza.
Hakuna matokeo rahisi kwa Simba kwenye mechi ya leo, kama Simba ilipata shida katika uwanja wa taifa ambao huweza kujinadi kwa samba lao basi bila shaka patakuwa pagumu katika uwanja wa CCM Kirumba leo.
Sina maana kuwa Simba itakosa pointi leo, hapana bali kwa jinsi mchezo wa soka ulivyo haitakuwa rahisi kama yalivyo matarajio ya mashabiki na wapenzi wa Simba.
Timu ya Simba inatakiwa kushuka uwanjani ikiwa na plani mbili au tatu tofauti hapa nina maana kuwa mbinu na maelekezo ya mwalimu wao ( Plan A) lakini pia plani B katika mchezo huo.

Comments
Post a Comment