April 13, 2017
Timu ya Simba imeshinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilimtumia nyota wake Mohamed Fakhi aliyekuwa na kadi 3 za njano kinyume na kanuni za ligi kuu.
Kamati ya saa 72 imejiridhisha kuwa Fakhi alioneshwa kadi tatu za njano katika mechi tatu tofauti ikiwemo dhidi ya Majimaji, Mbeya city na African Lyon.
Kamati hiyo imefikia uamuzi wa kurejesha pointi zote 3 kwa Simba baada ya kujiridhisha kuwa Kagera Sugar ilikiuka taratibu hizo.

Comments
Post a Comment