Timu ya Simba SC imepeleleka barua ya malalamiko TFF wakidai pointi 3 kutoka kwa Kagera Sugar wakihituhumu timu hiyo kumtumia Mohammed Fakhi ambaye alikuwa na kadi tatu za njano.
Katika rufaa hiyo, Simba imeilalamikia TFF kwa kitendo cha Kagera Sugar kumtumia Mohammed Fakhi kinyume na utaratibu wa kanuni za ligi kuu.
Kamati ya masaa 72 ya bodi ya ligi itakaa leo kupitia rufaa mbalimbali ikiwemo ya Simba dhidi ya Kagera Sugar.
Lakini kwa upande wa Kagera sugar Kocha wa timu hiyo Mecky Mexime amekanusha malalamiko hayo na kusema kuwa Fakhi alikuwa na kadi mbili za njano pekee.
Aidha Mexime aliongeza kuwa hivyo ni visingizio vinavyoletwa na timu hiyo baada ya Simba kupoteza ushindi wa mezani.

Comments
Post a Comment