Simba yamponza Eric Ngwengwe, atuhumiwa kuuza mechi Kirumba.


Timu ya Mbao FC imetangaza kumsimamisha golikipa wake Eric Ngwengwe kutokana tuhuma za kuuza mechi dhidi ya Simba SC katika uwanja wa CCM Kirumba.

Hayo yamesemwa na afisa habari wa timu hiyo Crinstant Malinzi ambaye amethibitisha kusimamishwa kwa Eric ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Golikipa huyo alichangia ushindi wa bao 3-2 ambao Simba ilipata kutokana na makosa ya wazi yaliyomuwezesha mshambuliaji Frederick Blagnon kuchomoa bao zote mbili.

Comments