Simba yatinga fainali kombe la FA.


Timu ya Simba imetinga fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuichapa Azam FC bao 1-0.

Bao la Mohamed Ibrahim aliyefunga dakika 48 ya mchezo huo ndiyo lililoipeleka Simba kwenye hatua ya fainali ya michuano hiyo.

Mfungaji wa bao hilo Mohamed Ibrahim ataukosa mchezo wa fainali baada ya kulimwa kadi nyekundu kutokana na kumfanyia madhambi Beki wa Azam Shomari Kapombe.

Mbali na kadi na nyekundu ya Mohamed Ibrahim pia Azam ilipata pigo kipindi cha kwanza baada ya Kiungo wao Sure boy kuoneshwa kadi nyekundu.

Comments