Sunderland yashuka daraja baada ya miaka 10.


April 29, 2017

Timu ya Sunderland imepoteza matumaini ya kuendelea na ligi kuu msimu ujao baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa AFC Bournemouth.

Bao la mshambuliaji wa Bournemouth Joshua King aliyefunga katika dakika 88 lilitosha kuisafirisha timu hiyo kwenye ligi ya championship.

Sunderland itakamilisha ratiba kwenye mechi tatu zilizobaki dhidi ya Hull city, Swansea na Arsenal.

Comments