Tanzania yapanda viwango vya FIFA.


Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imefanikiwa kupanda juu kwa nafasi 22 katika viwango vya soka vya kimataifa.

Taifa Stars iliweza kushinda michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Botswana na Buruni kwa mujibu wa kalenda ya FIFA.

Katika mechi ya kwanza Taifa Stars iliilaza Botswana kwa ushindi wa bao 2-0, pia iliichapa Burundi kipigo cha bao 2-1.

Stars imepanda kutoka nafasi ya 157 hadi nafasi ya 135 kutokana na kiwango kizuri cha soka ilichokionesha kwenye mechi za kirafiki.

Comments