Nahodha wa kipindi chote katika timu ya Chelsea tangu alipotua Jose Mourinho mwaka 2004 John Terry ameamua kuipa mkono wa kwa heri baada ya kudumu kwenye timu hiyo kwa miaka 22.
John Terry mwenye miaka 36 amedumu katika timu ya Chelsea tangu mwaka 1995 akitokea West Ham ya alipokulia tangu mwaka 1991 hadi 1995.
Mkongwe amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara ambayo yalipelekea kushuka kwa kiwango chake, na kuchangia makosa kadhaa katika siku za hivi karibuni.
Kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte ameonesha wazi kuwa John Terry hayupo kwenye mipango yake baada ya kumsajili David Luis kutoka PSG na wakati huu akimchungulia nyota wa Burnley Michael Keane.
John Terry amefanikiwa kunyanyua mataji muhimu akiwa na timu hiyo ikiwemo mataji ya ligi kuu English, FA, Capital one ambayo zamani ilifahamika kama Carlinga na taji la ligi ya mabingwa barani.
Pia Terry anashikilia rekodi ya kuwa beki aliyefunga mabao mengi zaidi katika ligi ya England ambapo hadi sasa amefunga mara 66.

Comments
Post a Comment