Toto yaikazia Simba CCM Kirumba.


April 15, 2017

Timu ya Toto Africans imeendelea kuitambia Simba ukiwa ni mwaka wa saba wekundu hao wameshindwa kupata ushindi katika uwanja wa CCM Kirumba.

Si Simba wala Toto Africans ambayo ilipata bao katika mchezo huo licha ya Simba kupata nafasi nyingi ikiwemo ile aliyoshindwa kuitumia Frederick Blagnon.

Simba imesonga mbele kwa alama 62 baada ya kugawana pointi na Toto Africans iliyosonga mbele kwa pointi 26 ikiendelea na kibarua cha kujikwamua isishuke daraja.

Matokeo hayo yanaweza kuwa Neema kwa timu ya Yanga ambayo huenda ikarejea kileleni na kuongoza msimamo wa ligi endapo itashinda mechi zake mbili zilizo mkononi.

Comments