April 28, 2017
Timu ya Tottenham Hotspurs itatumia uwanja wa kimataifa wa Wembley katika mechi zao za nyumbani msimu wa 2017/18.
Hatua hiyo ni kutokana na marekebisho ya yatakatofanyika katika uwanja wa White Hart Lane ambao unatarajiwa kupokea idadi ya watu 61000.
Hii si mara ya kwanza kwa Tottenham Hotspurs kutumia uwanja huo wa kimataifa wa England wenye kupokea idadi ya watu 90000.
Tottenham ilitumia uwanja ndani ya msimu huu katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kama uwanja wa nyumbani.
Tottenham itarejea kwenye uwanja wao wa awali katika msimu wa mwaka 2018/19 baada kumalizika kwa matengenezo ya uwanja wao.

Comments
Post a Comment