Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anavutiwa na mpango wa kumsajili kiungo wa Arsenal Mesut Ozil.
Mourinho aliwahi kumnoa mjermani huyo alipokuwa kocha wa Real Madrid akitokea Intermilan ya Italy.
Mourinho ameanza kuandaa mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa kiungo huyo ambaye amewahi kumpa mafanikio akiwa naye Real Madrid anatua Old Trafford.
Ikumbukwe Mourinho aliwahi kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Hispania kutokana na juhudi kubwa zilizokuwa zikifanywa na Mesut Ozil pale Santiago Bernabeu.

Comments
Post a Comment