April 18, 2017
Timu ya Brighton and Hove Albion inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England ndiyo inayoongoza kwenye harakati za kurejea ligi kuu (EPL) msimu wa 2017/18.
Brighton and Hove Albion ni moja kati ya timu kongwe inayopatikana nchini England ambayo ilianzishwa June 24, 1901 ikiwa imepita miaka 115 tangu kuanzishwa kwake.
Chris Hughton
Brighton ambayo inanolewa na Chris Hughton inaongoza msimamo wa ligi ya championship kwa pointi 6 mbele ya Newcastle United ambayo nayo inanukia ligi kuu England pia.
Mara ya mwisho timu hiyo kushiriki ligi kuu ilikuwa mwaka 1983 wakati huo ikiitwa "first division" baada ya kufungwa kwenye mechi ya mwisho na Manchester United.
Hughton ambaye amewahi kuzinona timu kadhaa England ikiwemo Newcastle, Birmingham City na Norwich anaenda kuandika historia mpya kwenye timu hiyo baada ya kuibuka shujaa.
Hadi kufikia jana ligi hiyo imebakiza michezo mitatu pekee lakini Brighton imekusanya jumla ya pointi 92 mpaka sasa ikifuatiwa na Newcastle yenye pointi 85 kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa pamona wakiwa na nafasi kubwa ya kutinga kwenye ligi ya EPL.
Wababe hao wanaopatikana kwenye jiji la Brighton and Hove Albion wamekuwa wa kwanza miongoni mwa timu mpya kabisa ambayo itakaribishwa ligi kuu msimu ujao tangu ilipoanza kuitwa ligi kuu England chini ya udhamini wa Barclays bank.
Timu ya Brighton imekuwa na mwenendo mzuri ilipoanza kunolewa na Chris Hughton tangu mwaka 2014 baada ya kuachia ngazi katika timu ya Norwich ambapo alionekana kuchemka.
Endapo timu hiyo itashinda michezo miwili ifuatayo itakuwa imejiahakikishia kuwa bingwa wa ligi hiyo lakini ikiwa na nafasi rasmi ya kurejea ligi kuu kutokana na wingi wa pointi ilizokusanya.


Comments
Post a Comment