April 23, 2017
Timu ya Yanga SC jana imehitisha rasmi orodha kamili ya timu nne zilizoweza kutinga kwenye nusu fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup baada ya kuichapa Prisons bao 3-0 katika uwanja wa Taifa.
Kuna hisia tofauti huenda Yanga na Simba zikakutana na kwenye hatua hiyo kusaka tiketi ya kuelekea kwenye hatua ya fainali ya michuano hiyo.
Mbali na Yanga, Simba pia Azam na Mbao zipo kwenye hatua hiyo wakisubiri hatma yao kuelekea April 28, mwaka huu ambapo michezo hiyo ya nusu fainali itaendelea.
Kwa upande wa Yanga kupitia kocha wao Juma mwambusi alisema kuwa hakuna timu wanayoihofia ikiwemo Simba ambaye ambaye ndiye mpinzani wake mkuu.
"Hatuna hofu na timu yoyote ikiwemo Simba, Azam na mbao, sisi ni mabingwa watetezi bado tunahitaji kulitetea taji letu na kulipeleka Jangwani kwa mara nyingine." Alisema Mwambusi
Lolote linaweza kutokea kwenye hatua hiyo nusu fainali na haitashangaza endapo watani wa jadi Simba na Yanga wakikutana kwenye hatua hiyo.

Comments
Post a Comment