Wenger aanza mipango mipya Arsenal.


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameanza kuweka mikakati mipya kwa ajili ya kikosi cha Arsenal msimu ujao.

Licha ya kupingwa na kuchokwa na mashabiki wa timu hiyo lakini Wenger atasaini miaka miwili kwenye mkataba mpya.

Wenger mwenye miaka 67 atasaini mkataba mpya muda wowote kuanzia sasa na inasadikika mkataba huo utawekwa mezani muda wowote kuanzia sasa.

"Ni kweli najiandaa na mipango mipya katika timu, msimu ujao nitakuwa hapa.

"Siwez kuzungumzia usajili kwa sasa, lakini Arsenal ni bidhaa kubwa ambayo inatambulika ulimwenguni kote." Alisema Wenger

Comments