Wenger kumwaga £200 milioni za usajili.


Kocha wa Arsenal, Arsenal Wenger yupo kwenye mipango ya kutumia kiasi cha Paundi 200 milioni kwa ajili ya kufanya usajili mkubwa kwenye timu hiyo.

Mbali na kutumia kiasi hicho cha usajili pia timu hiyo itawauza nyota wake kadhaa akiwemo Mesut Ozil, Oxlade Chamberlain, Jack Wilshere na Oliver Giround ili kuvuna kiasi cha £100 milioni kwa ajili ya kuongezea pesa ya usajili.

Arsenal imeandaa mipango kabambe ya kusajili nyota wakali wanaotamba kwenye medani ya soka akiwemo mshambuliaji wa Olympic Lyon Alexander Lacazzete na Moussa Dembele wa Celtic.

Pia Arsenal ipo kwenye mipango ya kumsajili beki wa kushoto Kierny Tierney ambaye anacheza Celtic na Winga wa Crystal Palace Wilfred Zaha.

Comments