Wenger: wala hatuna presha.


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema timu yake haina presha kuelekea kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Southampton usiku wa jumatatu.

Wenger alizungumza hayo na waandishi wa habari ambapo alisisitiza wanaangalia mbele na si matokeo waliyopoteza dhidi ya Crystal Palace.

"Kupitia wakati mgumu ni sehemu ya maisha pia, nadhani malengo ni kufanya maandalizi yaliyo bora kwa ajili ya mchezo uliyo mbele yetu.

"Matokeo ya mchezo wa soka huwa matatu, ukiwa katika soka unatakiwa kutarajia yote, wala hatuna presha akili ipo kwenye mchezo ujao." Alisema Wenger

Comments