Timu ya Yanga imeachia ngazi kwenye mashindano ya kimataifa hapo jana baada ya kupokea kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa MC Alger.
Kwenye hatua hiyo ya mtoano ya michuano ya kombe la shirikisho barani Africa, Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa nyumbani kwenye mchezo wa kwanza.
Lakini hapo jana mambo yalikuwa tofauti kwa upande wa Yanga ambayo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika ilikuwa imeshafungwa bao 2-0.
Rasmi Yanga imeaga mashindano hayo ambapo safari hii imeshindwa kutinga kwenye hatua ya makundi kama ilivyokuwa mwaka jana.

Comments
Post a Comment