Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa hautamzuia mchezaji yeyote anayetaka kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa Yanga Charles Bonifasi Mkwasa ikiwa no sehemu ya mikakati mipya ya timu hiyo.
Wapo wachezaji wanaomaliza mikataba yao ifikapo mwisho wa msimu huu akiwemo Vicent Bossou, Kevin Yondan na Nadir Haroub Cannavaro.
Yanga ambayo imeanza kujiandaa dhidi ya MC Alger ya Algeria imeanza kuweka mikakati mipya ya usajili kwa ajili ya kusuka kikosi imara msimu ujao.

Comments
Post a Comment