African Lyon, Toto na JKT Ruvu wameiaga ligi kuu.


May 20, 2017

Licha ya kuonekana kurudi vizuri msimu huu lakini timu ya African Lyon imeshindwa kumudu mikiki ya ligi na hivyo wamerejea ligi daraja la kwanza

African Lyon iliwabidi kushinda katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Tanzania Prisons lakini mchezo huo umemalizika kwa sare isiyokuwa na magoli.

Mbao FC imeshinda bao 1-0 dhidi ya Yanga na Ndanda imeshinda 2-0 dhidi ya JKT Ruvu na kulinda nafasi zao kwa pointi 33 kila moja.


Kali Mangonga Ongala anaonekana kuilewa vema Majimaji ambayo imesalia ligi kuu baada ya kupata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya mbeya na kusonga kwa pointi 35 juu ya Mbeya city, Ndanda na Mbao FC katika msimamo wa ligi kuu.

African Lyon, imeungana na JKT Ruvu pamoja na Toto Africans ambayo imechezea kichapo cha bao 3-1 katika uwanja wa Manungu dhidi ya Mtibwa Sugar.

Comments