May 17, 2017
Beki wa Manchester city Pablo Zabaleta amewaaga rasmi mashabiki wa timu hiyo baada ya ushindi 3-1 dhidi ya West Brom jana.
Zabaleta mwenye miaka 32, ataondoka kwenye timu mwisho wa msimu huu baada ya kuitumikia timu hiyo kwa muda wa miaka 9.
Mkataba wa beki huyo ambaye ni raia wa Argentina unamalizika rasmi mwisho wa msimu huu na hivyo hataongeza mkataba mwingine zaidi.
Zabaleta alianzia maisha yake katika ligi ya Spain ambapo mwaka 2008 alisajili Manchester city akitokea Espanyol.
Hadi sasa beki ameichezea city jumla ya mechi 232 na kutumbukiza bao 8 nyavuni.

Comments
Post a Comment