May 12, 2017
Mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC wanajindaa kuanzisha ligi ya vijana chini ya miaka 13 chini ya Azam mei 27 mwaka huu.
Michauano hiyo itahusisha timu kadhaa za vijana ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na kufanyika katika uwanja wa Azam Complex, Chamanzi.
Azam kupitia kupitia mkuu wa maendeleo wa soka la vijana Tom Legg alisema kuwa lengo la ligi hiyo kuniua na kuboresha maendeleo ya soka la vijana ili kupata wachezaji walio bora katika siku za baadae.
"Hii ni nafasi pekee ya kuinua na kuboresha vipaji kwa vijana, pia kuna nafasi kubwa ya kuniua na kunyanyua maendeleo ya soka katika nchi hii." Alisema Legg.
Ligi hiyo itahusisha timu sita za vijana ikiwemo Bom Bom SC, JMK Park Academy, Rendis FC, Ilala Academy, Magnet Youth na Azam.

Comments
Post a Comment