Azam: Tumejipanga vizuri kuifunga Toto Africa.


May 12, 2017

Timu ya Azam FC imesema kuwa imejipanga vizuri kuikabili Toto Africa katika mchezo wa ligi kuu leo kwenye uwanja Chamanzi Complex.

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa timu hiyo Jaffar Idd ambaye alithibitisha muungano mzuri wa mazoezi uliofanywa na kocha wa timu hiyo Aristica Cioaba kwa muda wa wiki nzima.

"Mwalimu amekiandaa kikosi vizuri kwa muda wa wiki tupo kamili kuikabili Toto Africans.

" Tunahitaji pointi tatu katika mchezo huo, ni muhimu kujihakikishia nafasi ya 3 msimu huu, ni lazma tupate pointi 3." Alisema Idd.

Comments