Barthez, Joshua hawana chao Yanga.


Golikipa wa timu ya Yanga Ally Mustapha 'Barthez' na beki wa kushoto wa timu hiyo Oscar Joshua wapo kwenye mipango ya kuondolewa kwenye kikosi cha Yanga kinachonolewa na mzambia George Lwandamina.

Barthez na Joshua wanatarajiwa kuungana na kocha wa wao wa zamani Hans Der Pluijm ambaye anakinoa kikosi cha Singida United.

Kwa pamoja wachezaji hao wamebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wao na timu ya Yanga na endapo hawatasajiliwa Singida United safari yao ndani ya Yanga itakuwa imefikia tamati.

Yanga ipo kwenye mikakati ya kuachana na baadhi ya wachezaji wakiwemo Oscar Joshua na Ally Mustapha ambaye amekuwa na makosa mengi uwanjani.


Comments