Cannavaro: Bahati haikuwa yetu


May 1, 2017

Beki wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amekiri kuwa imewauma kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa CCM Kirumba.

Cannavaro alisema kuwa licha ya kushambulia na kutawala zaidi mpira lakini bahati haikuwa kwao na hivyo wameshindwa kutetea taji lao.

"Nadhani tulicheza mpira mzuri, na tulishambulia sana langoni kwa Mbao lakini bahati haikuwa kwetu.

"Tumeumia sana kwa kushindwa kutetea ubingwa wetu kwa mara ya pili." Alisema Cannavaro.

Mbao FC itapata nafasi ya kushiriki Michuano ya kimataifa hapo mwakani endapo itashinda katika mchezo wa fainali dhidi ya Simba.

Comments