Chelsea haishikiki mbio za ubingwa England.


Timu ya Chelsea imeanza kunusa harufu ya ubingwa wa ligi kuu England baada ya kupata ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Middlesbrough katika uwanja wa Stamford Bridge.

Mabao ya Chelsea yaliwekwa nyavuni na Diego Costa aliyefunga dakika ya 23, Marcos Alonso dakika ya 34 na Nemanja Matic alihitimisha ushindi huo baada ya kufunga bao la 3 katika dakika ya 65.

Chelsea inahitaji kushinda mchezo mmoja kati ya mitatu iliyobaki ili iweze kutangaza ubingwa katika ligi hiyo.

Wakali hao wanaotamba na rangi ya 'blu' wanaongoza kwa pointi saba dhidi ya Tottenham Hotspurs ambayo ilipoteza ubingwa ndoto za ubingwa baada ya kupigwa bao 1-0 na West Ham.

Comments