Fainali kombe la FA kupigwa Dodoma.

Mei 2, 2017

Baada ya kuzagaa kwa taarifa za hapa na pale kuhusiana na uwanja utakotumika katika mchezo wa Fainali ya michuano ya kombe la Azam Sports Federation Cup hatimaye uwanja watajwa.

Fainali hiyo kati ya Simba SC na Mbao FC utapigwa katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Dodoma Mei 28, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF Simba ndiye atakayekuwa mwenyeji wa mchezo huo kutokana na kutangulia kufuzu kwenye hatua ya fainali katika nusu ya kwanza dhidi ya Azam FC.

Comments