Singida United imeendelea na harakati zake za usajili kwa ajili ya kujiweka sawa msimu ujao ambapo sasa wamehamia kwa wachezaji wa ndani.
Timu hiyo imeripoti kuwa ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na kiungo aliyetamba na kikosi cha Mbeya city Kane Ally ambaye alikuwa na msimu mzuri na timu hiyo.
Kane Ally alihusishwa katika kikosi bora ligi kuu msimu wa 2016/17 akiungana na nyota wengine ambao wameonekana kufanya vema katika soka.

Comments
Post a Comment