Beki wa kulia wa Taifa Stars Shomari Kapombe amesema kuwa hana mipango ya kucheza Tanzania ikiwemo Simba endapo ataondoka Azam FC
Kapombe aliyasema hayo kutokana na uvumi wa taarifa zinazomuhusisha beki huyo kujiunga na Simba SC kama ilivyo kwa John Bocco.
"Nafikiria zaidi kucheza nje ya nchi baada ya kumaliza maisha yangu ndani ya Azam, na wala siyo Simba au timu nyingine, kwa sasa nipo kwenye mazungumzo na Azam juu ya mkataba mpya." Alisema Kapombe.
Pia beki huyo aliongeza kuwa kitendo cha John Bocco kuondoka Azam FC ni jambo la kawaida katika maisha ya soka.
Comments
Post a Comment