Juve yaisubiri Real Madrid fainali.


Juventus ya Italy imekuwa ya kwanza kutinga fainali ya UCL baada ya kupata ushindi wa pili dhidi ya Monaco hapo Jana katika uwanja wa Turin.

Juventus ilipata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Monaco jana baada ya Dani Alves na Mario Mandzukic kuchungulia neti za Monaco katika kipindi cha kwanza.

Endapo Real Madrid atavuka kwenye hatua hiyo wababe hao watakuwa wamekutana tena fainali baada ya miaka 20.

Comments