Kocha wa England Gareth Southgate amesema kuwa amelazimika kumwondoa Rooney kikosini kutokana na uwepo wa nyota wenye kiwango zaidi yake.
Hayo yamesemwa na kocha huyo baada ya kujibu maswali kwa waliotaka kujua kwanini nahodha alitemwa ndani ya kikosi hicho.
"Nadhani wapo wachezaji na wenye kiwango kuliko Wayne Rooney, nadhani ni uamuzi sahihi kumuacha nyota huyo." Alisema Southgate.
England itacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Scotland na ufaransa ndani ya mwezi Juni ambapo Wayne Rooney hajahusishwa kwenye kikosi cha Southgate.

Comments
Post a Comment