Klopp asema Coutinho hauzwi popote.


May 11, 2017

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa hana mipango ya kumuuza nyota wa timu hiyo Felipe Coutinho.

Klopp alisema kuwa mipango yake kwa sasa ni kuongeza nguvu kwenye kikosi na si kupunguza nguvu kwa kuwauza nyota muhimu kwenye timu.

"Nili lini amesaini mkataba mpya? Ni siku za hivi karibuni nadhani tuna mipango ya muda mrefu na Coutinho.

"Malengo yangu ni kuunda kikosi imara, sina mpingo ya kuuza nyota wangu Muhimu." Alisema Klopp

Liverpool ina kibarua kizito cha kumlinda nyota wake kutokana na Barcelona kuonesha kiu ya kumuhitaji Coutinho mwenye miaka 24.

Comments