Lipuli FC ya Iringa ambayo imepanda daraja na itashiriki ligi kuu ya Vodacom msimu ujao imetanga kiasi cha shilingi milioni 800 za usajili.
Mwenyekiti wa timu hiyo Abduli Majeki amesema kuwa mbali na kiasi hicho cha fedha pia timu hiyo ipo kwenye mazungumzo na baadhi ya makampuni kwa ajili udhamini.
"Mbali na fedha hizo tulizotenga kwa ajili ya usajili, pia tupo kwenye mazungumzo na baadhi ya makampuni kwa ajili ya udhamini." Alisema Majeki.
Lipuli iliungana na Njombe Mji pamoja Singida United ambayo inatikisa kwa usajili baada ya kupanda daraja kwenye ligi ya Vodacom.
Comments
Post a Comment