Liverpool waikata maini Arsenal, waichapa West Ham 4-0


May 14, 2017

Matumaini ya Arsenal kurejea nne bora yanaonekana kukwama baada ya Liverpool kupata ushindi wa bao 4-0 dhidi ya West Ham katika uwanja wa Olympic.

Mabao ya Liverpool yaliwekwa nyavuni na mshambuliaji Daniel Sturridge, Phelipe Cotinho aliyefunga mara mbili na Divock Orogi aliyemaliza kazi kwa kutisa wavuni bao la nne.

Ushindi wa Liverpool huenda ukavunja moyo matumaini ya timu ya Arsenal kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya katika msimu wa 2017/18.

Liverpool inaongoza kwa pointi 4 juu ya Arsenal ambayo bado ina mchezo mmoja mkononi ikiwa na faida ya kucheza mchezo wa mwisho katika uwanja wa nyumbani.

Arsenal ina kibarua cha mwisho dhidi ya Sunderland katika uwanja wa Emirates na Everton katika uwanja wa Goodson park na kuitazamia Liverpool kupoteza mchezo wa mwisho.

Mechi ya mwisho kwa Liverpool dhidi ya Middlesbrough inaonekana kuwa unafuu tofauti na mchezo wa mwisho wa Arsenal dhidi ya Everton.

Comments